JUMAMOSI 20 FEBRUARI


Ilikua saa tatu za usiku. Tulilala mahala padogo, mwili wangu umeegezwa kwa ukuta ndio tutoshee kwa kitanda. Tuliongea juu ya siku yetu huku tukiskia milio ya popo wakiwa nje. Baada ya mda mchache nilihisi kuenda choo ambayo ilikua nje. Wenzangu walisema watiniunga.
Nje kulikua na giza totoro, hukuweza kuona hata pua chako. Mara tukasikia kelele kwa shamba ilio kando na hapo. Tulijua kwamba sisi ndio pekee tulio macho, huyu kwani ni nani? Haja ya kunipeleka choo ilipotea, huku nikishikilia tochi lisilokua na mwangaza tosha nilijaribu kubainisha ni nani aliyekua anatembea shambani wakati huu. Tulitulia tuli, mbwa iliyo karibu nanyumba yetu ilianza kubweka. Uoga ukatuzidi, tukaanza kutafuta njia ya kurudi kwa chumba chetu. Winston na Annette walikua nyuma yangu. Tulburutana kwa kasi tukijikwaa ili tufike haraka. Mwishoe tulifika salama, tukaingia ndani na kufunga mlango na kifuli alafu tukaweka mabagi zetu kuzuia mlango zaidi. Moyo wangu ulikua unapiga haraka huku nikijaribu kusikiza nje kuna nini. Baada ya mda mfupi tukasikia mtu nje na uoga ukazidi.



Wakati ulipita, nikitazama nje. Moyo bado wanidunda kwa uoga. Sikua najihisi niko salama, nikashinda nikiamsha Winston kujua kama amelala. Usiku huo sikupata hata lepe la usingizi.

Write a comment