JUMANNE, MACHI 9
Nimeishi kwenye kitongoji duni kwa wiki moja. Nahisi upweke lakini uoga wote umekwisha. Najaribu kuelewa utamaduni wao, fikra na maisha. Katika macho yao mimi niko tofauti na wao, lakini ukarimu wao umenipa furaha tele. Nimeanza kujihisi nyumbani mahala hapa. Kila siku mimi huja nyumbani na wao hutaka kujua jinsi siku yangu ilivyokua. Wao huuliza halafu wanataka kunipa mawaidha. Wanasema " Je, wajua kwamba filamu yako italeta majadiliano ya mada mbalimbali katika nchi"
Nimeaka saa 5:15 asubuhi. Watu wanne walikua wamesimama nje ya nyumba yangu. Nilijua kitu kibaya kimefanyika. Jirani yangu alikua anatoa machozi akilia. Nikauliza Joshua ni nini kinaendelea. Alinieleza kwamba mwenye analia alikua hajalipa kodi kwa muda wa miezi mitatu na alikua anaondolewa kwa nyumba.
Watu hao wanne walikua wanjaribu kutoa vitu vyake nje. Jirani huyo alikua mtu wa miaka 35 na alikua amefunga ndoa juzi. Hata hakufanya sherehe maanake hangeweza kuigharamia sherehe hio. Aliku pia anagharamia wazazi wake na wazazi wa mke wake. Na kuongezea hayo, alikua amepoteza kazi miezi mitatu iliyopita. Yeye hutafuta kazi kila siku, lakini kwasababu hana shahada zozote nafasi za kazi ni kidogo. Mke wake hufua nguo za majirani na watu wengine ili kupata fedha kidogo ya kodi na chakula. Lakini tulitatua tatizo hio ya kodi, ilhali si kwa muda mrefu.
Kama nilivyosema mbeleni, tunapitia mengi sana hapa. Jaribio kuu ni mahali pa kuoga mwili. Kila asubuhi sisi hupiga foleni kutupata nafasi ya kuoga. Unajaza ndoo yako, unabeba bilauri na kujimwagia maji na bilauri hiyo. Ukimaliza unajipangusa na leso.
Asubuhi mimi huanza siku hivi; naamka saa kumi na moja, nasafisha nyumba, naoga, nanywa kiamsha kinywa na Joshua, Winston na Annette. Kazi imezidi sasa. Nimeanza kazi kama mchongaji mbao. Joto na vumbi imezidi na inanifanya mchovu. Lakini najipa nguvu.
Write a comment