Jumatatu, Machi 15
Saa kumi na mbili asubuhi Joshua alibisha hodi nyumbani mwangu. Joshua ni mmoja wa watu watakao kuwa kwa filamu yangu na pi ni jirani yangu. Tangu nije Mombasa tumekua tunshirikiana kwa vitu vingi maishani. Amenisaidia sana kwa shughuli zangu za kila siku. Kwasababu ya hii, tumekua marafiki wa dhati, mshauri wangu na ninamheshimu sana. Lakini sisi hukosana wakati mwingine. Kwa vile asili zetu ni tofauti, yeye hupenda vitu vifanywe njia yake kwa kila kitu. Na mimi ni mjeuri siwezi kukubali hivyo kirahisi. Yeye huniambia kwamba nirekebishe tabia zangu ziwe kama za mwanamke wa asili ya kikenya.

Joshua husema kwamba mimi ni vigumu kusema "ndiyo" kwa mambo katika maisha ya kila siku. Jumapili iliyopita, alisema "Wewe husema "la" kabla hata nimalize sentensi yangu. Inabidi ushawishi mwingi ndio ukubali." Lakini kando na hayo, tunapenda urafiki wetu na vicheko hua vingi. Ni mtu mzuri mwenye roho safi na anasehemu kubwa ya kucheza katika mradi huu.

Kabla kutengeneza filamu, ni lazma uwe umeamua na kuamini wazo la filamu hiyo. Sehemu kubwa ni kuwa na watu walio na mawazo sambamba na wewe na wako tayari kujitolea asili mia moja kwa utengenezaji wa filamu hiyo. Nina furaha kusema kwamba watu nilionao ni watu wema na wenye mawazo kama yangu. Wamejitolea kwa kutengeneza filamu hii. Lakini mtu pia inafaa ajue anakosa Kufanikiwa. Leo, nikiangalia Anette na Winston naona kweli wameijtolea kwa kazi hii. Wanapitia mengi kama, magonjwa, uchovu, jasho, na kukasirika lakini bado wanajitahidi vyema. Shukran sana kwao na natumae bidii yao itafanya wengine wapate motisha ya kutoa zaidi.


Write a comment