Ijumaa, Machi 19
Siku hii tulisumbuka sana. Tulitaka kuenda Nairobi lakini hatukua na muda wa kuangalia ni jinsi gani tutafika huko. Baada ya kupigia watu kadhaa simu, tulipata taarifa kwamba tunaweza kusafiri na gari la moshi wakati wa usiku. Itatuchukua takriban masaa 12 kufika Nairobi. Tulipoenda kukata tiketi ya treni, tuligundua kua kulikuwa hakuna treni kutoka Mombasa hadi Nairobi siku ya Ijumaa. Tukafanya mabadiliko ya haraka kwa mipango yetu na kukata tiketi ya basi ya saa nne na nusu (10.30). Tulirekodi filamu siku ya mchana na kuenda kwa mikutano kadhaa.

Kutokana na kwamba tulilipishwa tiketi kwa bei ya juu, sisi tulidhani kwamba ilikuwa ni basi ya watalii na kwa hivyo hata watu kwenye basi watakua watalii. Ilipofika saa nne za usiku tulikua tumewasili kwa steji ya basi. Pole pole watu wakaanza kuingia ndani ya basi hilo na mda si mda tukaona kwamba ilikua sii basi ya watalii, lakini ya watu wa humu humu Mombasa. Watu walikua wamechanganyikiwa katika ile hali ya kutafuta viti vyao. Mimi nikakaa katika dirisha, Annette alikaa kando yangu, na winston kwa kiti iliyokua mbele yetu. Tulikaa tukitizama hali ilivyokua ndai ya basi hio. Watu walikua hawaelewani, mivurugano ilikua kila mahali. Annette nae aliamka na kujaribu kumsaidia mwanamke mmoja kutafuta kiti chake. Mwanamke huyo alipopata kiti chake, mhindi mmoja alijitokeza na kudai kwamba kiti hicho ni chake, ilhali kiti chake kilikua sicho. Waliongea baina yao kidogo alafu dereva wa basi hilo akaja kwa ukali na kumkejeli Annette akisema "Madam, najua basi langu". Annette alijaribu kumuelezea dereva huyo kwamba mhindi amekaa kwa kiti cha yule mwanamke, lakini dereva hakutaka kusikia, na mwanamke akepelekwa kiti kingine. Kwa ubaya, mwanamke huyo alikaa karibu na Annette, na akawa mwenye wa kuongea sana na sisi tulitaka kulalala kwasababu hatukua tumeona tone la usingizi kwa masaa mengi. Tulijikaza na mda mfupi baadaye tukapata kulala. Halafu tukasikia mlipuko BANG!!!...ilikua kama saa kumi kasorobo asubuhi. Tuliruka kwa uoga, miyoyo yetu inapiga kwa haraka kwa mshangao. Risasi ilikua imefyatuliwa kwa basi.
Kwasababu taarifa hii ni refu kidogo, nitaendelea kuwasimulia zaidi kuhusu mlipuko wa risasi kesho.
Write a comment