JUMAMOSI FEBRUARI 27
Leo ni siku kubwa kwangu. Ni siku yangu ya kwanza ndani ya nyumba ya Kiswahili. Katika vitongoji duni vya Mombasa, hhizi nyumba ndizo ziko nyingi. Hazina rangi, na zimejengwa na simiti na mabati, saa zigine hata na matope.
Unaingia nyumba kwa kupitia geti. Kwa sababu ya usalama, huwa kuna milango miwili au mitatu. Kila chumba kina mlango mmoja na dirisha moja. Kwa chumba hicho kidogo kunaa familia nzima. Vyumba hivi vya Kiswahili hushikilia watu hata ishirini ama thelathini. Choo na bafu ni moja na hutumiwa na kila mtu.



Ninakaa kwa chumba change nikingoja chakula - wali na mayai. Winston anashangazwa na jinsi nilivyotulia. Kichwa change kina mawazo mengi lakini Winston na Annette hawajui. Naogopa kwamba wakienda nitakuwa peke yangu. Kwamba itachukua mda kabla nizoeane na watu hapa. Lakini nikavumilia.





Write a comment