Nilikua na kutana na Rose saa kumi na moja kwa mkahawa. Sikua na matarajio yeyote. Nakumbuka nikiingia kwa mkahawa, nikamuona Rose, nikamsalimia na nikiwa navuta kiti nikae akarusha swali "Unataka kuja name Kenya kwa muda wa wiki mbili?"

Nilikaa kitako nimechanganyikiwa kwa madakika kadhaa. Nikaagiza kahawa na maswali yakaanza kunipitia kwa kichwa, "Tunaenda Kenya kufanya nini", "nitahitaji chanjo gani". Nilikua sijawahi kutembelea bara la Africa na nikaona hii ni nafasi ya kufanya ndoto yangu iwe. Nilikubali mara moja.
Tulionana siku ifuatayo na tukaanza kufanya mipango ya safari yetu ya Kenya. Nikafanya uchunguzi kuhusu nchi ya Kenya, mazingara yake, hali ya anga, makabila, siasa na umaskini. Ukifikiria kuhusu AfriKa mtu hufikiria samba, ndovu, vita, magonjwa, njaa na umaskini. Hata mimi nilifikiria hivyo tu.
Asubuhi iliyofuata tuliendelea na mipango. Rose alinieleza kinaga ubaga kuhusu mada ya filamu tuliokuwa tunaenda kurekodi. Alinieleza kua anataka kuishi kwa sehemu yenye umaskini zaidi Mombasa. Aliniuliza kama mimi ni mjasiri kufanya filamu hii. Nilikua na maswali mengi akilini. Sikua na uhakika kwamba mimi ni mjasiri wa kufanya kazi hio. Lakini pia nilitaka kujua kuhusu utamaduni wa Afrika na nafasi yangu ya kufanya hivyo ndio hii. Wiki mbili zilizofuata tulimalizia mipango yetu, na kupata chanjo zilizohitajika.

Sitasahau asubuhi hiyo tulivyokuatunaelekea kwenye uwanja wa ndege. Kulikua na barafu na theluji. Kichwani mwangu nilikua na fikira tele, ninaelekea Kenya, sio kama mtalii, lakini kama mpigaji picha wa filamu ya utamaduni wa Kenya na kujijulisha ju ya kabila ya wakamba.
Write a comment