Alhamisi Februari 18
Barabara ya kuenda wamunyu kutoka Nairobi ilikua na shimo tele. Mazingara lakini yalikua mazuri. Tulipata kuona milima, shamba za chain a mahindi. Tofauti kubwa na jiji la Nairobi. Hii ndio Kenya halisi, nilijiambia.
Tulikaribishwa vyema kwa nyumba ya Joshua, na Joshua akatuonyesha ng'ombe zake. Kulikua na nyumba za udongo kila mahali. Mahali hapa, wanawake ndio wana mamlaka. Mamake Joshua wa miaka 80 alikua anchunga ng'ombe huku akitafuta kuni. Maajabu.
Tulionyeshwa chumba chetu, choo kilikua cha nje kama yadi 30 kutoka nyumba yetu na ilikua choo ya shimo. Walikua wameweka majani kwa paa ya nyumba ili kufukuza popo usiku.
Kawaida huwa siogopi giza, lakini baada ya kuambiwa ju ya popo, nilitaka mwangaza wa jua uendelee wakati wote. Huku hawa maji wala stima. Jua ilipo potea, nilijihisi kama niko kwa dunia nyingine kwa sababu ya giza. Huko nyumbani Sweden, stima ipo kila mahali.
Usiku familia yote ilikusanyana na kula chakula cha jioni. Tulikaa karibu na Joshua akitueleza juu ya maisha yake ya utotoni huku Joshua akimtafsiria mamake ambaye alikua haelewi Kingereza. Maisha yao ni ya kawaida na nimependezwa nayo. Huku kuna hali ya amani. Baada ya mankuli Joshua alituonyesha mahali pa kulala.

Rose na Annette waliniangalia nikienda kulala kwa nyumba moja ya udongo. Walinicheka. Ndani ya nyumba hio hamkua na miti ya kufukuza popo. Najua utadhani mimi ni motto wa mama, lakini nadhani si wengi wangekubali kulala mahali pale.

Write a comment