Alhamisi Februari 18


Barabara ya kuenda wamunyu kutoka Nairobi ilikua na shimo tele. Mazingara lakini yalikua mazuri. Tulipata kuona milima, shamba za chain a mahindi. Tofauti kubwa na jiji la Nairobi. Hii ndio Kenya halisi, nilijiambia.


Tulikaribishwa vyema kwa nyumba ya Joshua, na Joshua akatuonyesha ng'ombe zake. Kulikua na nyumba za udongo kila mahali. Mahali hapa, wanawake ndio wana mamlaka. Mamake Joshua wa miaka 80 alikua anchunga ng'ombe huku akitafuta kuni. Maajabu.
Tulionyeshwa chumba chetu, choo kilikua cha nje kama yadi 30 kutoka nyumba yetu na ilikua choo ya shimo. Walikua wameweka majani kwa paa ya nyumba ili kufukuza popo usiku.
Kawaida huwa siogopi giza, lakini baada ya kuambiwa ju ya popo, nilitaka mwangaza wa jua uendelee wakati wote. Huku hawa maji wala stima. Jua ilipo potea, nilijihisi kama niko kwa dunia nyingine kwa sababu ya giza. Huko nyumbani Sweden, stima ipo kila mahali.
Usiku familia yote ilikusanyana na kula chakula cha jioni. Tulikaa karibu na Joshua akitueleza juu ya maisha yake ya utotoni huku Joshua akimtafsiria mamake ambaye alikua haelewi Kingereza. Maisha yao ni ya kawaida na nimependezwa nayo. Huku kuna hali ya amani. Baada ya mankuli Joshua alituonyesha mahali pa kulala.



Rose na Annette waliniangalia nikienda kulala kwa nyumba moja ya udongo. Walinicheka. Ndani ya nyumba hio hamkua na miti ya kufukuza popo. Najua utadhani mimi ni motto wa mama, lakini nadhani si wengi wangekubali kulala mahali pale.


Alhamisi februari 18


Tulikaa kwa Joshua, mji uliokua masaa matatu kutoka Nairobi. Mipango ilibadilika kidogo na ikabidi ni shughulike kujulisha serikali juu ya shughuli zangu za hapo kambiti.
Ilinikumbusha Sweden vile mtu akitaka huduma anazungushwa kutoka mahali moja hadi nyingine. Ni vile hatutaki kusghulikia jamii.


Tuliamua kufika Kambiti leo badala ya jana. Usiku ulijaa mvinyo, chakula na vicheko tukisherehekea mwanzo wa mradi wetu.




Tulikuja kwa njia ilio na shimo nyingi. Lakini mazingira yalikua mazuri sana. Kulikua na furaha tele nilipoonana na Joshua na Julius. Mwisho kuwaona ni kama mwaka moja uliopita. Sasa tumepata kuonana tena. Kulikua na mbuzi wengi, ng'ombe, na kuku. Tuliweza kusikia mbwa ikibweka huko nje na tukaona paka zikizurura kila mahali. Kulikua hakuna stima, maji wala joto. Nilijiuliza ni vipi wanaishi wakati wa baridi. Choo ni tofauti kabisa na ile ya nyumbani mwangu. Ni choo cha shimo na shimo yenyewe ni ndogo zaidi hadi nikashtuka vipi nitakavyoitumia.
Leo tulishinda na Joshua na Julius na familia zao tukizunguka mtaa wao. Tulitrekodi kidogo na tukafanya mkutano mdogo alafu tukalala.



KUHUSU KAMBITI: NI kijiji katika eneo la wamunyu, nyumbani mwa kabila ya wakamba. Huku kuna misitu, na milima mengi. Boma la wakamba huwa na nyumba kadhaa za mawe ama tofali na paa huwa mabati. Nyumba nyingi hazina maji wala stima. Watu wa huku huongea kikamba, lakini waliobahatika kuenda shule huongea pia Kiswahili na kiingereza.

Kabla ya kuweka ujumbe mpya, ningependa kufafanua jambo moja, ujumbe zote ni za wakati uliopo. Sababu ya kufanya hivyo ni kwamba Winsston na Mimi tuliandika kuhusu safari hii kila siku. Tulikua Kenya kuanzia Februari had Machi mwaka wa 2010. Nitazidi kuweka tarehe ndio uweze kufuata safari yetu vyema. Tuko Sweden Kwa sasa, lakini kuna hadithi nyingi nitawaeleza karibuni.



Tumewasili Kenya na tunaweza kuanza kurekodi filamu yetu.
Wiki mbili zilizopita zimekua ngumu. Hata sikua na wakati wa kumuaga mpenzi wangu. Safari ilikua njema, sote tulilala kwa ndege. Winston alisaidia mtu moja asigongwe na mwanamke mwingine kwa ndege. Siwezi kukueleza vile kulikua lakini Winston alisaidia. Safaari ya ndege ilikua refu, tulisimamia mji wa Istanbul. Mji huo una kiwanja ndogo ya ndege.



Tuliwasili Nairobi saa 03.30 asubuhi. Kulikwa na joto jingi na nje kulikuwa na giza na kumenyamaza. Mchana ulipofika nilikuwa na tamaa ya kutoka na kuzunguka Nairobi.


Mpango tuliokuwa nao ilikua kuenda kijiji cha Kambiti ambayo ilikua masaa 2-3 kutoka Nairobi na kukutana na Julius na Joshua. Lakini kwanza ilibidi tuende kutafuta idhini ya kuruhusiwa kurekodi filamu Kenya. Hatutakua na wakati wa kupumzika lakini natumae tukifika nyumbani kwa Joshua tutalala unono.


Nilikua na kutana na Rose saa kumi na moja kwa mkahawa. Sikua na matarajio yeyote. Nakumbuka nikiingia kwa mkahawa, nikamuona Rose, nikamsalimia na nikiwa navuta kiti nikae akarusha swali "Unataka kuja name Kenya kwa muda wa wiki mbili?"



Nilikaa kitako nimechanganyikiwa kwa madakika kadhaa. Nikaagiza kahawa na maswali yakaanza kunipitia kwa kichwa, "Tunaenda Kenya kufanya nini", "nitahitaji chanjo gani". Nilikua sijawahi kutembelea bara la Africa na nikaona hii ni nafasi ya kufanya ndoto yangu iwe. Nilikubali mara moja.
Tulionana siku ifuatayo na tukaanza kufanya mipango ya safari yetu ya Kenya. Nikafanya uchunguzi kuhusu nchi ya Kenya, mazingara yake, hali ya anga, makabila, siasa na umaskini. Ukifikiria kuhusu AfriKa mtu hufikiria samba, ndovu, vita, magonjwa, njaa na umaskini. Hata mimi nilifikiria hivyo tu.
Asubuhi iliyofuata tuliendelea na mipango. Rose alinieleza kinaga ubaga kuhusu mada ya filamu tuliokuwa tunaenda kurekodi. Alinieleza kua anataka kuishi kwa sehemu yenye umaskini zaidi Mombasa. Aliniuliza kama mimi ni mjasiri kufanya filamu hii. Nilikua na maswali mengi akilini. Sikua na uhakika kwamba mimi ni mjasiri wa kufanya kazi hio. Lakini pia nilitaka kujua kuhusu utamaduni wa Afrika na nafasi yangu ya kufanya hivyo ndio hii. Wiki mbili zilizofuata tulimalizia mipango yetu, na kupata chanjo zilizohitajika.



Sitasahau asubuhi hiyo tulivyokuatunaelekea kwenye uwanja wa ndege. Kulikua na barafu na theluji. Kichwani mwangu nilikua na fikira tele, ninaelekea Kenya, sio kama mtalii, lakini kama mpigaji picha wa filamu ya utamaduni wa Kenya na kujijulisha ju ya kabila ya wakamba.