November 2010

Jumamosi, 20 Machi




Safari yote ya kuelekea Nairobi tulikua macho kama popo. Tulikua hatujalala kwa masaa 29 na hatujakula kwa masaa 16. Tulipokua tunaelekea Masai mara niliona kweli tumekuwa wavumilivu. Mlipuko wa risasi ulikua haututatizi tena. Ilitusumbua tu dakika kama thelathini baada ya kuusikia mlipuko huo. Katika safari hii tumekuwa mashujaa kama wanajeshi. Tulivumilia mengi na wakati ukizidi kuenda, na matukio yakiongezeka, tulizidi kua wavumilivu. Rafiki yangu mmoja wa dhati aliniandikia na kuniambia kwamba anaona safari hii imenibadilisha sana. Tumeona mengi hapa Kenya. Tumepata hisia nyingi tofauti ambayo hatukudhani yapo. Tunashukuru kwa yale ambayo tunayo. Nchi hii imetuathiri kwa njia nzuri. Kila siku ni kama miaka mengi. Nilianza kuogopa kurudi Sweden manake sikujua vile safari hii imeniathiri na vile watu nyumbani watanichukua.

 

 


Tukielekea Masai Mara: Jua ilikua kali zaidi tulihisi tuko jikoni. Miguu na migongo yetu ilikufa ganzi. Tulikua tumekaa kwa gari kwa mda wa masaa manne na hapakua na afasi ya kunyorosha miguu. Nilianza kupoteza uvumilivu wangu. Niliona kama hatutawahi kuhitimu lengo letu. Niliambia dereva asimame, nikafungua mlango wa gari na nikashuka. Sikufikiria nilichokua nafanya mpaka nilioanza kukumbuka mahali nilpokua. Kulikua na wanyama wa pori wengi kama chui na simba katika mahali hiyo. Pole pole nilirudi kwa gari na kuingia, huku nikishukuru kuwa ndani na si nje ya gari.



Masaa mawili baadaye tulifika kwa lango la Masai Mara. Askari wawili walitukujia.......mengi zaidi kesho.



 

Bibi ya Joshua na Rose

 

 

Majirani wa Rose

 

 

Winston na Joshua

 

 

Jua ikipaa chaani

 

 

Msichana Kanisani

 

 

Mtu aliyetusaidia kufungua soda

 

 

Kanisani

 

 

Rose na wanawake wa chaani

 

 

Mtoto wa rafiki yetu

 

 

chaani

 

 

chaani

 

Nitawacha Winston aendelee na Hadithi:


Ijumaa 19 Machi


Mwanamke aliyetuwekea viti vya basi alituuliza "Mna hakika mnataka kutumia basi?". Alikua kama mama aliye na wasiwasi kwasababu ya watoto wake. Wakati huo nilikua nimechoka na joto na nilitaka tu tuondoke.


Mlipuko ulinamsha saa tisa za asubuhi. Nilikua nimelala huku nikiegeza kichwa kwenye kioo cha basi. Mlipuko ulipotokea, nilisikia glasi ziniangukia kwa nyuso. Sikuelewa kilichokua kinatendekea. Nilikua nimeshtuka huku nikiona shimo kwa kioo cha basi. Nilijiangalia mwili kama nilikua nimeumizwa kokote, mara nikaskia Rose na Anetten wakiniambia " weka kichwa chini Winston". Nilijirusha chini ju ya glasi ziliokua zimenguka chini. Dereva wa basi naye akapeleka basi kwa kasi ili kuondoka mahali hapo.


Nilikaa chini kwa dakika chache alafu nikasongea mahali Rose na Annette walikua wamekaa. Nilishangaa vile watu wengine kwa basi waliku watulivu ni kama hakuna kilichotendeka.
Haikuwa mpaka jioni tulipokua Masai Mara ambapo nilielewa kilichotendeka. Dereva wetu alitueleza kwamba ilikua ni watu wanajaribu kuiteka nyara basi hio. Sikua bado naweza kuamini kwamba niliku karibu na kupigwa risasi. Nilinyamaza huku nikivumta pumzi na kushukuru kwa mashia niliyo nayo.


Ijumaa, Machi 19


Siku hii tulisumbuka sana. Tulitaka kuenda Nairobi lakini hatukua na muda wa kuangalia ni jinsi gani tutafika huko. Baada ya kupigia watu kadhaa simu, tulipata taarifa kwamba tunaweza kusafiri na gari la moshi wakati wa usiku. Itatuchukua takriban masaa 12 kufika Nairobi. Tulipoenda kukata tiketi ya treni, tuligundua kua kulikuwa hakuna treni kutoka Mombasa hadi Nairobi siku ya Ijumaa. Tukafanya mabadiliko ya haraka kwa mipango yetu na kukata tiketi ya basi ya saa nne na nusu (10.30). Tulirekodi filamu siku ya mchana na kuenda kwa mikutano kadhaa.



Kutokana na kwamba tulilipishwa tiketi kwa bei ya juu, sisi tulidhani kwamba ilikuwa ni basi ya watalii na kwa hivyo hata watu kwenye basi watakua watalii. Ilipofika saa nne za usiku tulikua tumewasili kwa steji ya basi. Pole pole watu wakaanza kuingia ndani ya basi hilo na mda si mda tukaona kwamba ilikua sii basi ya watalii, lakini ya watu wa humu humu Mombasa. Watu walikua wamechanganyikiwa katika ile hali ya kutafuta viti vyao. Mimi nikakaa katika dirisha, Annette alikaa kando yangu, na winston kwa kiti iliyokua mbele yetu. Tulikaa tukitizama hali ilivyokua ndai ya basi hio. Watu walikua hawaelewani, mivurugano ilikua kila mahali. Annette nae aliamka na kujaribu kumsaidia mwanamke mmoja kutafuta kiti chake. Mwanamke huyo alipopata kiti chake, mhindi mmoja alijitokeza na kudai kwamba kiti hicho ni chake, ilhali kiti chake kilikua sicho. Waliongea baina yao kidogo alafu dereva wa basi hilo akaja kwa ukali na kumkejeli Annette akisema "Madam, najua basi langu". Annette alijaribu kumuelezea dereva huyo kwamba mhindi amekaa kwa kiti cha yule mwanamke, lakini dereva hakutaka kusikia, na mwanamke akepelekwa kiti kingine. Kwa ubaya, mwanamke huyo alikaa karibu na Annette, na akawa mwenye wa kuongea sana na sisi tulitaka kulalala kwasababu hatukua tumeona tone la usingizi kwa masaa mengi. Tulijikaza na mda mfupi baadaye tukapata kulala. Halafu tukasikia mlipuko BANG!!!...ilikua kama saa kumi kasorobo asubuhi. Tuliruka kwa uoga, miyoyo yetu inapiga kwa haraka kwa mshangao. Risasi ilikua imefyatuliwa kwa basi.
Kwasababu taarifa hii ni refu kidogo, nitaendelea kuwasimulia zaidi kuhusu mlipuko wa risasi kesho.


Jumatano, Machi 17


Ilikua siku ya sherehe. Tulihisi furaha kwasababu tulipata nafasi ya kutulia na kupumzika kidogo. Winston aliku anasherehekea siku yake ya kuzaliwa. Tulifanya kazi siku nusu pekee alafu tukaamua kwamba tutaenda kwa nyumba yangu ya kiswahili kusafisha na kuaandaa chakula cha mchana. Lakini baada ya kufikiria kidogo, niliona aibu kuwapeleka huko na nikawashawishi tuende kwa hoteli yao.



Tulikula chakula kizuri hotelini, na nikajihisi mtalii kweli. Nilihisi kama niko kwa dunia nyingine tofauti kutoka ile ninayo ishi mimi. Tulimalizia usiku kwenye vilabu katika eneo la mtwapa, ambapo tulijiunga na marafiki wetu wa zamani wa Kenya, George,Zero, Mike na Paul. Usiku ulikua wenye furaha, kucheza dansi, na vichekesho vingi. Kuishi Kenya kweli ni kuzuri. Kila kitu huku kinafanywa kwa ustadi. Ukiwa mzungu huku, unapendwa sana. Wakenya wanajua wanachotaka na ni wastadi kwa kufuata kitu hicho wakitakacho. Wanajaribu sana kunipa mistari ya mapenzi. Tulifurahi sana na tukakutana na watu tele, lakini cha muhimu ni kwamba tulipata nafasi ya kupumzika kidogo.