November 2010

Jumanne, Machi 16


Ilhali sisi hufanya kazi masaa ishirini kila siku, saa zingine sisi hukaa na kuongea ju ya yale tunayoyaona na kupitia hapa. Wakati mmoja, Anette alikua na maoni haya:



"Ni kama kuna mstari inayotutofautisha sisi (wazungu) na wakenya. Najaribu sana kuonyesha kama sioni haya matatizo. Mimi nina shibe na nguo safi. Na kuna watoto wadogo nawaona na nguo zilizoraruka na chafu. Kuna taka kila mahali, na nyumba zimejengwa kwa udongo na mabati. Wanakaa kama hawana usaidizi wowote. Hii sii haki. Maisha yao imenifanya nione kama natoka kutoka dunia tofauti"



Siku chache zilikua zimebaki na singeweza kulipia chakula hotelini ama kuenda kujifurahisha kwa kilabu. Sikuweza kununua hata nguo ama chochote ninachokihitaji. Lakini tarehe 25, pesa iliingia kwa akaunti yangu, na nikaweza kununua vitu nilivyohitaji na kulipa madeni. Mbeleni, sikuelewa maisha yanaweza kua hivi.


Anette: "Huko ng'ambo nina nyumba iliyo safi na yakupendeza. Nina friji iliyojaa vyakula vingi, nina bafu kubwa iliyo na maji safi inayotoka kwa mferiji. Lakini kwa nyumba ya Rose ya kiswahili, ana sahani moja, na hamna maji kwa bafu. Maji inanunuliwa kwa mitungi na ni ghali sana. Nikiangalia vile Rose anaishi, vile ambavyo majirani wake wanaishi watu hata saba kwa chumba moja ndogo, naona masikitiko sana. Hata watu wakiniambia nafaa kuishi kwa matajiri, naona ni kweli. Kuona umaskini wa hali hii umenitatiza sana. Nimekua nikiona kwa runinga lakini kamwe sikua nimeona na macho yangu."



"Najua pesa, nguo na vitu vya duniani sio kila kitu maishani. Najua sasa kwamba mapenzi na urafiki ni bora kuliko chochote kengine. Lakini kwangu mie, sio pesa ama nguo ambayo ndio shida. Shida yangu ni kupenda starehe. Serikali ya nchi hii imeshindwa kuwalinda watu wao kutoka umaskini. Macho yangu imefunguliwa. Najiona ni kama nimelindwa na wavu ya usalama na sina matatizo ya maisha. Nikifikiria watu wanoishi na Rose, naona kweli hawana mlinzi wa kuwachunga, hawana wavu wa usalama."




Jumatatu, Machi 15


Saa kumi na mbili asubuhi Joshua alibisha hodi nyumbani mwangu. Joshua ni mmoja wa watu watakao kuwa kwa filamu yangu na pi ni jirani yangu. Tangu nije Mombasa tumekua tunshirikiana kwa vitu vingi maishani. Amenisaidia sana kwa shughuli zangu za kila siku. Kwasababu ya hii, tumekua marafiki wa dhati, mshauri wangu na ninamheshimu sana. Lakini sisi hukosana wakati mwingine. Kwa vile asili zetu ni tofauti, yeye hupenda vitu vifanywe njia yake kwa kila kitu. Na mimi ni mjeuri siwezi kukubali hivyo kirahisi. Yeye huniambia kwamba nirekebishe tabia zangu ziwe kama za mwanamke wa asili ya kikenya.




Joshua husema kwamba mimi ni vigumu kusema "ndiyo" kwa mambo katika maisha ya kila siku. Jumapili iliyopita, alisema "Wewe husema "la" kabla hata nimalize sentensi yangu. Inabidi ushawishi mwingi ndio ukubali." Lakini kando na hayo, tunapenda urafiki wetu na vicheko hua vingi. Ni mtu mzuri mwenye roho safi na anasehemu kubwa ya kucheza katika mradi huu.



Kabla kutengeneza filamu, ni lazma uwe umeamua na kuamini wazo la filamu hiyo. Sehemu kubwa ni kuwa na watu walio na mawazo sambamba na wewe na wako tayari kujitolea asili mia moja kwa utengenezaji wa filamu hiyo. Nina furaha kusema kwamba watu nilionao ni watu wema na wenye mawazo kama yangu. Wamejitolea kwa kutengeneza filamu hii. Lakini mtu pia inafaa ajue anakosa Kufanikiwa. Leo, nikiangalia Anette na Winston naona kweli wameijtolea kwa kazi hii. Wanapitia mengi kama, magonjwa, uchovu, jasho, na kukasirika lakini bado wanajitahidi vyema. Shukran sana kwao na natumae bidii yao itafanya wengine wapate motisha ya kutoa zaidi.


 


Jumapili, Februari 14



Mda unazidi kuyoyoma, na kila siku mambo mapya yanajitokeza. Ndio maan nina hisi kama nimeishi Kenya miezi mingi. Kila siku majaribio ni mengi. Leo ni jumaili na kama kwaida ni siku ya kuenda kanisisani. Majirani wangu wamejivalia nguo zao za kupendeza. Saa nne kamili inatupata tumekaa katika kanisa ambayo Joshua na Julius huenda. Baada ya nyimbo kadhaa, michezo ya kuigiza na dansi, mhubiri alianza kuhuburi neno. Alisema maneno mazuri na jinsi alivyokua anaongea ilisisimua watu. Lakini kanisa yenyewe haikua vyema. Masikio yangu ilijaribu kubainisha kati ya maneno na kelele. Mimi ni mtu anayehangaika sana, na katika hali kama hiyo nachoka kwa urahisi na nahisi kuwa mgonjwa. Na kuongeza chumvi kwa kidonda, mhubiri alionge kwa Kiswahili, lugha nisichokielewa. Ilibidi nivumilie sana nisilie kwa mahangaiko. Winston alijaribu kwa uwezo wake kunipiga picha lakini hata yeye alikua anahangiaka. Baada ya masaa mawili Winston aliniuliza, " Kwani Kanisa hii haikwishi?". Ilikua tayri ni saa saba mchana. Namgeukia Joshua nikijaribu kadri ya uwezo wangu nisilie nikamuuliza "kanisa yaisha saa ngapi?" akanijibu " saa kumi". Nilimweleza Winston na hakuamini masikio yake. Hatangeweza kufanya lolote na kwa hivyo tuka kaa na kusikiza. Baada ya masaa mangine matatu kanisa ilikwisha na nikajihisi mshupavu wa kuvumilia yaote hayo.


 


Mahojiano ya Jana yalitupa uchovu mwingi sana. Tulijaribu kutafuta takwimu ya kuvutia kuhusu maisha ya mhusika mmoja katika filamu yetu. Lakini pia, isingekuwa vyema kujihususha sana na maisha ya mhusika huyo kwasababu hatukua na uwezo wa kumsaidia. Hii ndio changamoto ambayo tunapambana nayo kila siku.



Ijumaa, Machi 12


Kama Kawaida, Joshua alibisha mlangoni mwangu saa kumi na moja asubuhi. Kichwa kilikua kinaniuma. Leo nilikua niamke, nile kiamsha kinywa, ni fanye mazoezi, nisafishe, nifagie, nioga na nijitayarishe kwa kazi ya filamu. Winston alikuwa tayari amewasili mahala pa kupigia filamu ya leo. Changamoto nilioona isio ya kawaida ni kwamba nitapigia mswaki asubuhi na nijioni huko akamba handicraft. Harufu kutoka kwa choo na bafu ya mahala ninapoishi hunifanya kuhisi mgonjwa.



Nasikia kuchoka. Mwili umejaa uchovu lakini pia niko na motisha. Leo nimesumbuliwa na nimechoka. Naona haya kukubali nimechoka kwasababu nataka niwe na uwezo wa kushughulikia kila kitu, niwe mwenye nguvu na uvumilivu. Najiona kama ndege ambae anawaeleza watu zaidi mia moja ninaokutana nao kilia siku nini ninafanya na kwanini. Nimechoshwa na watu kwa njia kuniita mzungu. Naumia kwasababu ya kuona umaskini na shida ya wakenya. Uchungu moyoni haushi na huzuni imenijaa. Poleni wakenya kwa matatizo yenu. Sasa nahisi kama ni ndugu zangu na siwezi kuwaacha wakiteseka. Leo niliku na donda la koo kwa kushuhudia haya lakini lazima nitimize nilichokusudia kufanya. Hisia zangu zinanieleza kwamba siku moja nitwasaidia hawa. Nimetamani niwe na familia yangu, nile chakula cha mamangu. Nawapa hongera nyie mnaoishi kwa shida ya harufu mbaya, uchafu, joto, ajali barabarani umaskini, hasira, utamaduni usioleta maendeleo na ufisadi. Na yote haya kwasababu hamna nafsi nyingine.



Nitakuja nyumbani usiku. Majirani wangu huwa wamekaa katika yadi. Mimi nitajiunga nao. Huruma yao, upendo na udadisi unanitia nguvu. Kuona dunia katika macho yao ni shida, lakini jamii yao, jinsi ambavyo wanahudumiana.



JUMANNE, MACHI 9


Nimeishi kwenye kitongoji duni kwa wiki moja. Nahisi upweke lakini uoga wote umekwisha. Najaribu kuelewa utamaduni wao, fikra na maisha. Katika macho yao mimi niko tofauti na wao, lakini ukarimu wao umenipa furaha tele. Nimeanza kujihisi nyumbani mahala hapa. Kila siku mimi huja nyumbani na wao hutaka kujua jinsi siku yangu ilivyokua. Wao huuliza halafu wanataka kunipa mawaidha. Wanasema " Je, wajua kwamba filamu yako italeta majadiliano ya mada mbalimbali katika nchi"


Nimeaka saa 5:15 asubuhi. Watu wanne walikua wamesimama nje ya nyumba yangu. Nilijua kitu kibaya kimefanyika. Jirani yangu alikua anatoa machozi akilia. Nikauliza Joshua ni nini kinaendelea. Alinieleza kwamba mwenye analia alikua hajalipa kodi kwa muda wa miezi mitatu na alikua anaondolewa kwa nyumba.
Watu hao wanne walikua wanjaribu kutoa vitu vyake nje. Jirani huyo alikua mtu wa miaka 35 na alikua amefunga ndoa juzi. Hata hakufanya sherehe maanake hangeweza kuigharamia sherehe hio. Aliku pia anagharamia wazazi wake na wazazi wa mke wake. Na kuongezea hayo, alikua amepoteza kazi miezi mitatu iliyopita. Yeye hutafuta kazi kila siku, lakini kwasababu hana shahada zozote nafasi za kazi ni kidogo. Mke wake hufua nguo za majirani na watu wengine ili kupata fedha kidogo ya kodi na chakula. Lakini tulitatua tatizo hio ya kodi, ilhali si kwa muda mrefu.


Kama nilivyosema mbeleni, tunapitia mengi sana hapa. Jaribio kuu ni mahali pa kuoga mwili. Kila asubuhi sisi hupiga foleni kutupata nafasi ya kuoga. Unajaza ndoo yako, unabeba bilauri na kujimwagia maji na bilauri hiyo. Ukimaliza unajipangusa na leso.
Asubuhi mimi huanza siku hivi; naamka saa kumi na moja, nasafisha nyumba, naoga, nanywa kiamsha kinywa na Joshua, Winston na Annette. Kazi imezidi sasa. Nimeanza kazi kama mchongaji mbao. Joto na vumbi imezidi na inanifanya mchovu. Lakini najipa nguvu.